Ashika sehemu nyeti za ajuza, aburuzwa kortini kujibu mashtaka

 Aisee wahenga wa kale hawakukosea waliposema,ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Jamaa mmoja mwenye umri wa makamu alishtakiwa mbele ya korti ya Kiambu kwa kosa la kujaribu kumbaka nyanya yake mtaa wa Banana wiki mbili zilizopita.

Michael Karanja Wairimu,jina lake mshtakiwa,alisimama mbele ya korti ya kiambu na kupewa adhabu na hakimu Stella Atambo kwa makosa ya kutaka kushiriki ngono na nyanya yake bila idhini ya ajuza huyu.

Vilevile,inasemekana kuwa siku hiyo alishika sehemu nyeti za ajuza huyu kwa kutumia mikono yake.

Hata hivyo,bwana Karanja alikataa madai haya na kuachiliwa baada ya kulipa fidia ya shilingi elfu mia moja (100,000) na kesi yake kusikizwa tarehe tatu mwezi wa January mwaka ujao. (3/1/2020).

Zaidi ya hayo,mkubwa wa milki wa kikao bwana Donnex Ongira alisema kuwa ana mashahidi watano tayari ambao wako tayari kuwa mashahidi wa kesi hiyo.

Katika korti hiyo hiyo,jamaa mmoja jina lake Bernard Mungai alishtakiwa kwa kumnajisi binti wa miaka 11 tarehe 20 mwezi wa Oktoba.

Mbali na hayo,bwana huyu alishtakiwa kwa kosa la kushika sehemu nyeti za mtoto huyu bila idhini yake.

Hata hiyvo,jamaa huyu alikataa mashtaka yote na hakimu akamuweka huru  baada ya  kutoa faini ya shilingi elfu 200,000.

Kesi ya jamaa huyu itatajwa tarehe 6/01/2020.