Iwapo ulidhani Diamond Platnumz ni mmiliki wa WCB, basi soma upekuzi huu!

ROMY-AND-DIAMOND-4
ROMY-AND-DIAMOND-4

Jina Wasafi Records (WCB) si geni sana hususan kwa wapenzi wa miziki ya Bongo na mashabiki wa Diamond  Platnumz, Harmonize na wengineo.

Sallam ambaye ni meneja wa Diamond wakati moja aliandika katika mtandao wake wa Instagram ujumbe ulitoa mwanga kuhusu mmliki asili wa  WCB.

Ujumbe wake ulisoma hivi :

“BREAKING NEWS: SAA MOJA KAMILI USIKU WA LEO NAKUJA NA MAKALA MAALUMU NAOMBA MUWEKE BANDO, NA SIMU FULL CHARGE, NOTIFICATION ON. #YALIYOFICHWAYATAFUKULIWALEO #TUMEKATAAKUWAKAA”

Hata hivyo baadaye alishurutishwa kutotoa taarifa hizo za upekuzi.

Hapo awali,  Diamond na wasimamizi wa idhaa ya Clouds FM hawajakuwa na uhusiano mwema na meneja huyo alitaka kutumia fursa hii kulipiza kisasi lakini Joe Kusaga ambaye anadaiwa kuwa mojawapo wa wamiliki wa WCB aliwazuia kutoa taarifa hizo.

Hii ni baada ya kubaini kwamba mfanyabishara mwenza Ruge Mutahaba ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Clouds Fm alikuwa miongoni mwa waliopanga hiyo njama ya kulipiza kisasi.

Na hili kutuliza na kupoza na kutuliza mambo Sallam alituma ujumbe mwingine uliosema hivi:

“Kwa heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye  industry ya muziki. WCB haina tatizo naClouds Media Group ila Ruge Mutahaba ndio tatizo# Tumekataakuwaka.

Hata hivyo inaaminika kwamba ngome hiyo na ya kurekodi muziki nchini Tanzania inamilikiwa na  Joe Kusaga na Ruge Mutahaba.