Utani wa Janet Mbugua kwake Hussein Mohamed, asimulia mshangao huo

Hussein-and-Janet-696x418
Hussein-and-Janet-696x418
Msomaji habari Hussein Mohamed amesimulia baadhi ya matukio yaliyomvutia na kabisa hawezi kusahau kipindi anafanya na runinga ya Citizen.

Kumbukumbu hizi zilichezwa katika runinga ya Citizen kama ishara ya kukumbuka siku za awali.

Kilichomwacha kinywa wazi ni tukio la Janet Mbugua kumtania kuwa tendo la kujifungua mtoto wake Huru lingemjia mubashara akisoma habari.

"Tukio hilo lilinitia hofu sana..."
"Nitazungumzia swala hilo siku nyingine..."

Kumbukumbu za Hussein zinatokea baada ya mwanahabari huyu kutangaza kujiuzulu.

Hussein alikuwa anasoma habari katika kituo hicho pamoja na kufanya mijadala na mahojiano.

Mohamed amekuwa akisoma habari kwa kipindi cha miaka 10.

Hussein alitangaza taarifa hizi kupitia mtandao wa Twitter.

“Imekuwa miaka 10 ya kufana sana katika kituo cha Citizen. Nimefurahia na kujihisi freshi na wafanyakazi wenzangu…”

“Nimeamua nichukue breki kidogo baada ya Oktoba ili niangazie maswala mengine…’ ulisoma ujumbe wake wa Twitter.

Kutoka kwake kunafuatia kujiuzulu kwa Janet Mbugua ambaye alisema anatoka kufanya dili za kibinafsi.

Mashabiki na wafuasi wake wamemtakia mema baada ya uamuzi huo.