Nilipata kondomu kwa nyumba - Bwana Fred apasua mbarika

massawe
massawe
Nina swali kwenyu mlio kwenye uhusiano au kwenye ndoa.

Hebu fikiria, wewe unaishi pamoja na mpenzio na wewe hufanya inayohitaji kusafiri mara kwa mara. Siku moja ukirejea nyumbani unapatana na mipira ya kondomu, je utafanya nini?

Hiyo ndiyo ilikuwa hali kwa jamaa kwa jina Fred aliyepasua mbarika jinsi hali hiyo ilivyomharibia ndoa yake.

Akizungumza na mtangazaji, Massawe Japanni Fred alieleza kuwa hapo awali alikuwa anafanya kazi Nairobi kabla ya kwenda Meru. Siku moja aliporudi nyumbani alipatana na mpira wa kondomu na makaratasi yake.

Isitoshe, mkewe alikiwa nyumbani na baada ya kuuliza kuhusu yale, majibu ya mkewe hayakumfurahisha na aliondoka na kurudi Meru. Zimeoita miezi mitatu na bado hana nia ya kurudi.

Soma uhondo wote,

Mimi nimekaa kwa ndoa miaka mitano, sasa unajua kabla mwaka wa tano kuisha nilikuwa nafanya kazi Nairobi na nikarudi Meru. Niliporudi kwa nyumba kutoka safarani nilipata mpira wa kondomu.

Aki ya mungu niligoroka (kutokwa na wazimu) Niliipata chumbani pamoja na hayo makaratasi yake, nilishikwa na wazimu hata sijawahi enda huko tena na nikawachana na huyo mwanamke kabisa.

Niliuliza maswali na nikashindwa nitafanya nini sasa labda wananchi wanipe ushauri nijue mtu hufanya nini akikumbwa na maneno kama hayo.

Ilikuwa miezi mitatu iliyopita na mama hupiga simu lakini mimi hukata kwa sababu ya kisirani tu.

Nilipomuuliza aliniambia kuwa alikuwa amepeana nguo yake kwa mwanamke mwingine na labda alikuwa anatoa kitu mfukoni na ikaanguka.