Upekuzi: Paul Manyasi aliyedondoka kwenye KQ na Cedric Shiunja ni mmoja

Kisa cha mwanaume aliyedondoka katika ndege ya KQ Julai kimekuwa cha kukanganya sana hususan baada ya familia inayokisiwa kuwa ya jamaa huyo kukana madai hayo huku wakisema mwanao ni Cedric Shiunja.

Mwili wa Paul Manyasi ulioganda kutokana na kupigwa na upepo mkali uliangukia bustani moja nchini Uingereza wakati ndege ya KQ ilipofungua magurudumu yake ikijiandaa kutua.

Hata hivyo haijabainika wazi iwapo Manyasi aliaga dunia katika safari hiyo iliyochukua masaa manane na nusu au alifariki alipoangukia ardhi mkavu.

Kulingana na upekuzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Sky News, inaonesha kwamba Manyasi alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Colent iliopewa kandarasi ya usafi katika uwanja wa ndege wa Nairobi.

Hata hivyo, kampuni ya Colnet ambayo ilipinga madai hayo huku ikikana kuwepo kwa mfanyakazi kwa jina la Paul Manyasi.

Jamaa huyo anaaminika kujificha katika gurudumu la ndege katika angatua ya JKIA Nairobi.

Babake Isaac Manyasi katika mahojiano na kituo cha KTN alisema kwamba mwanawe yupo katika rumande na hakuwa amefariki jinsi ilivyoripotiwa.

"Si mwanangu, niliwaambia walionionesha kwenye picha sio kijana wangu, mwanangu hajakuwa nyumbani tangu 2016 alipoenda Nairobi," Isaac alisema.

Awali, familia ilisema kuwa mwana wao ni Cedric Shiunja wala sio Paul Manyasi.

Aidha, iliongezea kuwa hawajui mwanao alipo na wamekataa taarifa za kuhusishwa na mwili wake Paul.

Hata hivyo, upekuzi wetu unatudhihirishia kwamba Cedrick na Paul ni mamoja.

Kakake mkubwa Paul pamoja na mke wake Janet wanasema hawajapata kumsikia kutoka kwake Paul tangu Julai.

Ikumbukwe kwamba Paul Manyasi alidondoka kutoka ndege ya KQ mnamo Julai 2, 2019.

Kulingana na mitandao yao kijamii, tulibaini haya:

(i) Alisomea chuo kikuu cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT).

(ii) Alienda shule ya upili Tande.

(iii)Anaishi Naiorbi South, Nairobi Area, Kenya.

(iv)Anatoka Kakamega.

Picha zilizotumiwa na Sky News zilimtambulisha Paul Manyasi kuwa sawa na picha za Cedrick zilizokuwa kwenye mtandao wa kijamii.

Hizi ni baadhi picha zake: