(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi kadhaa mwilini anaendelea kupata afueni katika hospitali ya KNH (Kenyatta National Hospital).

Jamaa huyu alipigwa risasi na majambazi wawili waliovamia duka mtaa wa Kasarani viunga vya jiji kuu la Nairobi.

Katika kipande cha video kilichosambaa kama moto wa nyika mitandaoni, Richard alipiga mmoja wa majambazi hao katika juhudi za kuokoa mwenye duka.

Kwa sasa mmewe bado yupo katika sehemu ya watu mahututi wanaohitaji usaidizi wa haraka zaidi.

Mkewe amesema kuwa anawashukuru zaidi madaktari wa hospitali hiyo.

Familia imejotolea kutoa usaidizi katika hali hii ngumu.