Matokeo ya KCPE hayamfurahishi kamwe, afika nyumbani kupata ndugu walikufa

Anna-1-696x361
Anna-1-696x361
Huku idadi kubwa ya wanafunzi ikisherehekea matokeo ya KCPE yaliyotangazwa jana na waziri George Magoha, Anna Zambi hana furaha yoyote.

Msichana huyu ambaye ni raia wa Tanzania alizama katika hali ya mawazo baada ya kupata wanafamilia walifariki wote.

Watu wa ukoo waliweka usiri mkubwa sana ili asiweze kufahamu kifo chao.

Anna alikuwa akiwasubiri wazazi pamoja na ndugu zake wamtembelee siku ya maombi kabla afanye mtihani wa KCPE ila hakuna aliyetokea.

Anna,16 hakujua wazazi na ndugu zake waliaga dunia wote.

Familia ya Ann ilihusika katika ajali na kufariki.

Gari yao ilisombwa na maji katika eneo la Handeni mkoa wa Tanga, Tanzania.

Kulingana na mipangilio ya wanafamilia, walitaka wamfahamishe kuhusu kisa hiki pindi akimaliza mtihani wake wa KCPE.