Jamaa aruka kutoka feri ya MV Harambee na kujirusha bahari Hindi Likoni

EKJMk6OX0AAFFLc
EKJMk6OX0AAFFLc
Maafisa wa polisi mjini Mombasa wanachunguza kisa na ambapo mwanaume aliruka kutoka kwa feri ya MV Harambee na kutumbukia ndani ya maji ya bahari Hindi.

Kisa hiki kilichofanyika Jumamosi kinakisiwa kuwa jaribio la kujiua huku mwili wa marehemu ukisalia ndani ya maji.

Wengi wanahisi kuwa mwanamme huyo alikuwa na matatizo ya akili yaliyotokana na kuzongwa na fikra.

Jamaa huyu ambaye hajatambulikana aliruka kutoka sehemu ya nyuma ya MV Harambee.

Sio mara ya kwanza watu wasiojulikana kujirusha katika bahari.

Kwa mujibu ya kauli iliyotolewa na shirika la feri nchini,feri hiyo alikuwa inavuka kutoka vuo za Hindi kwenda katika kisiwa.

Juhudi za kutafuta mwili huo zinaendelea.

Picha zilizonaswa na kamera za CCTV zinaonyesha kuwa jombi huyu alitoka kwenye kiti na kuruka baharini.

"Alikuwa amevaa shati nyeupe na suruali nyeusi. Aliacha kiti chake na kujirusha.Tunatuma pole zetu kwa familia iliyoathirika..."Shirika la Feri lilichapisha Twitter.