''Joho aligharamia wimbo wa Ring,'' Kelechi Africana afunguka (+video)

collage-1-11
collage-1-11

Mwanamuziki Kelechi Africana kutoka nchini kenya haswa jijini Mombasa amejulikana sana kwa wimbo wake 'Ring' uliosambaa na kuwafurahisha wengi.

Katika mahojiano na Mpasho,mwanamuziki huyu alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa gavana wa Mombasa bwana Hassan Joho aligharamia wimbo wake wa 'Ring' ambao umefanya vyema sana katika mitandao ya kijamii.

‘RING WAS COURTESY OF 001, HE FUNDED IT.

I DID NOT KNOW HOW MUCH HE CONTRIBUTED BECAUSE WHEN YOU FOLLOW TOO MUCH YOU WILL EITHER LOOSE OR SOMETHING ELSE WILL HAPPEN.'' Kelechi alisema.

Zaidi ya hayo,mwanamziki huyu alisema kuwa alikutana na Mheshimiwa wakati wa kampeni za kule Mombasa alipojaguliwa kuimba katika kampeni zile.

 Licha ya hayo,Kelechi alipoulizwa alijihisi vipi aliposkia kuwa wimbo wke unabobea sana alisema kuwa,alishtujka sana na hata hakuwa anatarajia kuwa wimbo wake utapendwa hivyo.

Ama kwa hakika Mungu akisema atakubariki hakuna atakayezuia.