Mwanaume aliyempiga mlinzi wa lango mtaani Komarock akamatwa -Video

Justin Kamoja
Justin Kamoja
Mwanaume aliyenaswa kwenye kanda ya video akimdhulumu mlinzi wa lango kwenye mtaa wa Komarock, Narobi ametiwa mbaroni.

Kulingana na maafisa wa DCI, mwanaume huyo anayetambulika kama Justus Kamoja mwenye umri wa miaka 30, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Katika kanda ya video hiyo, Kamoja anaonekana akimsukuma mlinzi huyo kwa fujo na kisha kufungua lako kuu na kutoka na gari lake.

Alifungua lango hilo kwa nguvu bila ruhusa kutoka kwa mlinzi wa mtaa.

Dhuluma hizo kutoka kwa Kamoja zimemtia mashakani na kwa sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Afisi ya upelelezi wa makosa ya jina kupitia mtandao wa twitter umepongeza umma kwa kujitokeza na kukashifu tukio hilo.