Sanura Sandra ahamia kwa Tanasha kumlea Naseeb Junior

Screenshot_from_2019_11_28_09_21_52__1574922150_73217
Screenshot_from_2019_11_28_09_21_52__1574922150_73217
Sanura Sandra ametangaza kuwa ana mipango ya kuhamia nyumbani kwa Tanasha ili kusaidia kumlea mtoto Naseeb Junior.

Hii ni baada ya sherehe kubwa kufanyika kwa ajili ya mtoto.

Sherehe hizo ambazo ziliandaliwa katika jumba la kifahari la Diamond, Madale katika mji mkuu wa Dar es Salaam, zilikuwa za kusheherekea siku 40 tangia kuzaliwa kwa mwanao, Naseeb Junior.

Wawili hao walichukua fursa hiyo ya kipekee ya kuonyesha waliouhudhuria sura ya mtoto huyu kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na gazeti la Global Publishers nchini humo, Sandra amesema kuwa atamuacha mumewe kwa muda ili kutoa msaada wa kumsaidia mama Tanasha kumlea Naseeb Jnr.

Mastaa wengi walialikwa Madale ili kusherehekea sherehe ya siku 40 tangu mtoto azaliwe.