(+ Video) Visanga vya BBI na nyufa za Jubilee, Ruto akiombea ripoti ya BBI

Screenshot_from_2019_11_30_12_08_36__1575106947_82098
Screenshot_from_2019_11_30_12_08_36__1575106947_82098
Matukio ya picha na vipande vya video katika hafla ya kuwasilisha ripoti ya BBI yanaonyesha nyufa kubwa kati ya naibu wa rais William Ruto na rais Uhuru Kenyatta.

Tayari chama tawala kina migawanyiko miwili, TangaTanga na Kieleweke.

Tazama video inayoonyesha Dennis Itumbi akifurushwa ukumbi wa Bomas.

https://twitter.com/TheRealBBI_Ke/status/1199771986781704193

TangaTanga ni kikundi na ambacho kinahusisha viongozi wanaomzingira Ruto huku kikisheheni wanasiasa kutoa bonde la ufa na pia ngome ya Uhuru.

Tazama hapa naibu wa rais William Ruto akiombea ripoti ya BBI.

https://twitter.com/BKhaniri/status/1198631021782196227

 Kieleweke kina wabunge kutoka vyama vya upinzani na Jubilee wanaounga mkono BBI na 'Handshake' ya Raila Odinga na Uhuru.

Katika hafla hiyo iliyofanyika siku chache nyuma, wabunge wa TangaTanga wakiongozwa na Murkomen wanahoji kuwa kuna njama fiche ya kugeuza mapendekezo ya BBI kupitia mlango wa nyuma.

Tazama video ya maafisa wa usalama wakimzuilia Ruto nje ya kikao cha Uhuru na Raila.

https://twitter.com/KelvinWaKarimi/status/1200488402388475905

Murkomen alilalama kuwa mpangilio wa wazungumzaji katika hafla hiyo ulilenga kuwanyamazisha waliokuwa na mchango badala wa maoni.

Vituko vilivyoendelea katika hafla hiyo ni wazi kuwa nyufa za wanachama wa Jubilee ni pana mno.

Kwanza, Itumbi kutimuliwa katika jukwaa aliyokuwa rais na viongozi wengine mbele ya kamera za wanahabari.

Pili, Ruto kufungiwa nje katika kikao cha Raila na Uhuru.

Tatu, wabunge wa TangaTanga kutopata nafasi ya kutoa mchango wao kuhusu mapendekezo ya BBI.