Je ni haki? Kocha wa Enugu FC afutwa kazi kwa njia tatanishi

Katika kitengo cha kila siku asubuhi cha story za Ghost ambacho huletwa kwako na Ghost Mulee, mtangazaji huyo husimulia visa ambavyo vimekuwa vikitendeka humu nchini na duniani kote.

Hii leo, Ghost alisimulia kisa ambacho kimeongelewa na wengi, haswa mashabiki wa kadanda duniani.

Inadaiwa kuwa kocha mmoja nchini Nigeria, wa timu ya Enugu FC, alifutwa kazi kwa njia tatanishi baada ya timu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

Akisimulia Ghost, ambaye pia yeye aliwahi kuwa kocha, alisema kuwa kocha huyo kwa jina, Benedict Ugwu, alifutwa kazi huku mechi yao dhidi ya Akwa starlets ikiendelea, na isitoshe kupitia kipaza sauti.

Jambo hilo liliwashtua na kuwakera wana Nigeria ambao waliwakemea wasimamizi wa timu hiyo kwa kufanya uamuzi huo ambao haukuonesha heshima.

Tukio hilo pia lilimkumbusha Gidi wakti ambapo hapo nchini, kocha mmoja wa Gor Mahia alilazimishwa na mashabiki kujiuzulu.

Skiza usimulizi wake Ghost Mulee,

&feature=youtu.be