Watu watano wafariki dunia kutokana na mlipuko wa volkano

New zealand Volcano
New zealand Volcano
Watu kadhaa wameokolewa katika mlipuko wa volkano uliotokea nchini New Zealand.

Jumla ya watu takribani 35 walinusurika bila majeraha huku wengine 30 wakiendelea kupata matibabu katika hospitali mbali mbali nchini New Zealand.

Zaidi ya watu watano waliaga dunia kutokana na mlipuko huo huku wanane hawajulikani waliko.

Miongoni mwa waliokuwa wakipata matibabu ni raia wawili wa Uingereza kulingana na afisi ya kamishina mkuu wa Uingereza iliyoko New Zealand.

Waziri mkuu wa AustraliaScott Morrison anasema kuwa raia wake 24 walikuwa katika ziara ya utalii kwenye kisiwa  cha Bay of Plenty mlipuko wa volkano ulipotokea.

Kulingana na shirika la BBC, wahasiriwa wa mkasa huo waliokolewa kwa boti na helikopta.

Aidha linasema kuwa juhudi za uokoaji zinakumbwa na hali mbaya ya miundo msingi, moshi na jivu kutoka volkano.