Uchokozi na kejeli za Diamond Platnumz kuhusu fiesta ya Ali Kiba

Screenshot_from_2019_12_13_01_50_55__1576219884_68287
Screenshot_from_2019_12_13_01_50_55__1576219884_68287
Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz ameonekana kufurahia tamko la bosi wa runinga ya Clouds Joseph Kusaga kuwa fiesta alizofanya kwa kipindi kirefu hazijaleta faida yoyote.

Akihojiwa katika kipindi cha BarTender kinachoruka kupitia runinga inayomilikiwa na Diamond, Kusaga amefunguka kuwa sio vizuri kushindanisha ukumbwa wa vyombo vya habari nchini humo.

https://www.instagram.com/p/B57wL1JpHi-/

"Naomba nikwambie kitu kimoja. Mimi ukichukulia fiesta niliyofanya, haijawaji kunipa faida kwa miaka yote unaweza ukakataa..." Allisema Kusaga.

Ikizingatiwa kuwa msanii Ali Kiba utumbuzia katika matamasha haya ya Clouds, Diamond ilibidi atoe kauli.

"Wenyewe wanasemaga BABA KASEMA...Jamani haka Kamsemo kuna sehemu kanaingiaga Utamu bwana...." Aliposti Mondi kwenye Insta.

Mastaa hawa wawili wamekuwa katika bifu huku mashabiki wao wakiwa katika makundi mbalimbali ya kuwaunga mkono.

Fiesta la Wasafi kwa mara nyingi limeshindanishwa na fiesta la runinga ya Clouds.