Mike Mbuvi Sonko kufunguliwa kesi mpya Voi

sonko
sonko
Mike Mbuvi Sonko anatakiwa kujiwasilisha mahakama ya Voi Jumatano tarehe 18 Disemba ili kujibu mashtaka dhidi yake.

Sonko anadaiwa kumjeruhi afisa wa polisi wakati na ambapo alikuwa anatiwa nguvuni na makachero wa EACC.

Upande wa mashtaka unahoji kuwa kiongozi huyu alimpiga na kumshambulia Bwana Rashid Yakub.

Mashtaka mengine ni sawa na kuvunja kamera za wanahabari pamoja, kutoa cheche za matusi na kuwatatiza wanapolisi kutekeleza kazi yao.

Kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Haji aliagiza Sonko afike mahakama hiyo ya Voi baada ya kesi hiyo kuwasilisha katika ofisi yake.

"Wakati wa kutiwa nguvuni, (Sonko) alitoa matusi na rabsha alipokuwa akikataa kutiwa mbaroni na kuwazuia maafisa wa polisi kutekeleza kazi yao kisheria," kauli ya polisi ilisoma.

"Katika harakati hizo, alimshambulia na kumjeruhi afisa wa polisi aliyekuwa akiongoza kikosi cha polisi na pia kuharibu vifaa vya wanahabari," kiliandikwa kipande cha taarifa za polisi.