Vifo vya wasanii maarufu nchini ambavyo vilituacha vinywa wazi

Sekta ya burudani imekuwa na wakati mgumu miaka michache ambayo imepita kufuatia vifo vya wasani maarufu humu nchini.

Hawa ni baadhi ya watu maarufu ambao wameyapoteza maisha yao.

Jastorina

Nancy Nyambura aliyejulikana kwa jina lake la utani, Jastorina, alikuwa mwigizaji kwa kipindi cha 'the funny house help' aliiaga dunia mwaka wa 2014.

Alifariki kutokana na ugonjwa wa meningitis aliokuwa nao kwa muda mrefu.

Aliwaacha wavulana wake wawili.

Salim Junior

Alipendwa na wakubwa kwa wadogo kwa nyimbo zake mashuhuri alizoziimba kwa lugha yake ya mama.

Salim aliyeitwa Paul Mwangi, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Nakuru Memorial ambapo alikuwa anapokea matibabu.

Kulingana na familia yake, alikuwa anaugua kwa muda mrefu.

Alifariki mwezi wa Agosti mwaka wa 2018.

Ayeiya

Emmanuel Makori Juma aliyejulikana kwa jina lake la utani kama Ayeiya alipatana na kifo chake mwezi wa Aprili mwaka wa 2018.

Alikuwa akielekea nyumbani baada ya kurekodi maagizo yake pale Canivore ambapo ajali ilifanyika katika barabara ya Langata karibu na chuo kikuu cha CUEA.

Big Kev

Big Kev alifariki baada kupigana muda mrefu na saratani ya ubongo.

Big Kev alipatikana na ugonjwa huo mwaka wa 2010 na kufariki tarehe 29 mwezi wa Julai mwaka wa 2017 katika hospitali ya Nairobi alipokuwa amelazwa mwezi wa Februari mwaka wa 2017.

Jina lake kamili lilikuwa Kevin Ombajo.

Maureen Wanza

Maureen Wanza alicheza mchezo wa kuigiza 'Sumu' na alijulikana kama Sasha.

Wanza alikutana na kifo chake mwaka wa jana mwezi wa Septemba alipokuwa anajifungua, mtoto wake alifariki katika harakati hiyo pia.

Jamal Gaddafi

Jamal Gaddafi alifariki mwaka jana.

Aliuwawa na mpenziwe.