James na mkewe wa miaka zaidi ya 20 walilazimika kutengana baada ya mke huyo kuanza kumpa mateso ya kimawazo kwa kumfanya kelele na pia kuwa na uhusiano wan je ya ndoa na naiu wa chifu na hata afisa mmoja wa polisi . Njenga anasema wakati wa ndoa yake ,wakati mmoja mkewe alitoroka na kumwacha na mtoto wao aliyekuwa na miezi mitano . Anasema lengo lilikuwa kumfanya aondoke ndiposa mkewe aichukue mali yake .Amesimulia jinsi kipande chake cha ardhi kilivyozwa na mkewe katika jitihada za kumwacha mikono mitupu .
Njenga anawashauri wanaume kuwa na ujasiri wa kuweza kusema wazi kwamba wanapitia mahangaiko katika ndoa zao ili waweze kusaidiwa .kwa sasa Bwana Njenga alianzisha shirika lisilo la kiserikali ili kuwapa usaidizi wanaume wanaopitia mateso katika ndoa . Alipoafika mwisho na kuchoka na mateso haya yote Njenga alioa mke wa pili ambaye wameishi naye kwa miaka tisa sasa bila matatizo .