kesi ya mauaji ya mwendazake George Muchai kuskizwa, Januari 28, 2020

Ni mauaji ya utata ambayo ilitokea mnamo tarehe ,7,mwezi wa pili 2015,mauaji ambayo yalisababisha kifo cha mwenda zake George Muchai aliyekuwa kua mbunge wa Kabete,dereva wake na walinzi wake wawili waliokuwa kwenye doria siku hiyo.

Jana hakimu Roseline Oganyo aliweza kuamuru keshi hiyo iweze kuendelea tareehe 28 Januari 2020.Huku akisisitiza mashahidi nane wa mwisho waweze kuwa katika mahakama wakati wa kesi hiyo.

Walioshtakiwa ni Eric Isabwa almaarufu mwenyekiti,Raphael Kimani almaarufu Kum Butcher,Mustapha Kimani almaarufu Musto,Stephen Astiva almaarufu Chokore,Jane Wanjiru almaarufu Shiro,Margaret Njeri na Simon Wambugu waliweza kukataa madai kumi ya wizi wa mabavu.

Katika mahakama ya juu washukiwa hao waliweza kushtakiwa kwa mauaji ya mbunge Muchai, walinzi wake wawili, Samuel Kailikia, Samuel Matanta na dereva mmoja aliyefahamika kama Stephen Wambugu mnamo tarehe ,7,Februari 2015.

Mauaji hayo yalitokea katika barabara ya Kenyatta Avenue Nairobi.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo washukiwa hao wameshtakiwa kwa wizi wa mabavu ambapo dada hao wawili ambao ni walalamikaji walidai kuwa walikuwa wametekwa nyara muda mfupi kabla ya mauaji ya mbunge George Muchiri.

Dada wa mbunge huyo pia ni shahidi katika kesi hiyo itakayo endelea 28 januari mwaka huu.

Mbunge huyo alipigwa risasi na mwanaume mmoja ambaye alikuwa amesema kuwa mke wake yuko hatarini kabla ya mauaji hayo.

Kulingana na mashtaka mwanaume huyo aliweza kutoka katika gari ambalo liliweza kupita gari laa mwendazake Muchiri kwa mwendo wa kasi katika eneo la jumba la Nyayo CBD mnamo saa tisa za mchana tarehe ,7,februari 2015.

Mbunge huyo alikuwa anaelekea nyumbani kwake baada ya sherehe ya familia iliyokuwa katika kilabu cha Galileo mtaa wa Westlands Nairobi.

Ilisemekana kuwa mshukiwa mkuu ambaye alimpiga risasi Muchai aliweza kuwa na wasaidizi wawili ambao waliwanyang'anya walinzi wa Muchai bunduki zao na kuchukua mfuko ambao walikuwa nao na kisha kuendesha gari lao kwa kasi.

Ni mauaji ambayo hayajaweza kujulikana kwanini yalitokea, swali ni je washukiwa hao wataweza kuchukuliwa hatua mwafaka kwa kitendo hicho ama wataweza kuhukumiwa kifungo cha maisha?