Mulee abubujikwa machozi akisimulia masaibu ya wachezaji (VIDEO)

Hapo jana, mtangazaji, Ghost Mulee aliwashangaza wafuasi wake na mashabiki kwa jumla alipochapisha video katika mtandao wa Instagram, akitokwa machozi.

Kwenye video hiyo, Mulee anaonekana akiwa ndani ya gari lake usiku na kulingana na sauti yake ni kama alikuwa amelia kwa muda.

Anaanza kwa kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye sio mlevi ila ameguswa na tukio moja ambapo mama kwa jina Sarah alimtumia bili ya 740 ya chakula, bili ambayo ni ya wachezaji saba walioko katika chuo cha soka cha Liberty.

Mulee amekuwa akigadhabishwa na visa vya wachezaji kukosa kulipwa marupurupu yao huku lengo lake likiwa kuinua mchezaji mwingine atakaye inua hadhi ya nchi hii kama Michael Olunga.

Aliwarai wakenya kuanza kuwashika wachezaji mkono na kuwekeza kwa vijana kwani hao ndio tegemeo letu la kesho.

Alisema,

Sarah wa academy amenitumia bill hapa sahii ananiambia vijana wako leo wamekula 740, 740 ni nini? 740 kenyan shillings for 7 players. I sacrificed that to make the next Olunga.

I am sad there are millionaires in this country they invest in b…sh*t. Please invest in our youth because they are the future.

I want Kenya to be in the World Cup in 2026 please just invest in a player.

Tizama kanda hii,

https://www.instagram.com/p/B7oePL9F5BV/