‘Ni Uchungu’: Willis Raburu aeleza ugumu wa maisha baada ya kumpoteza mtoto wake .

rABURU
rABURU
Mtangazaji  Willis Raburu ,ni mtu mcheshi sana na mwingi wa kila kizuri cha kumpa yeyote tabasamu .Lakini  ameyapitia ya kumpa chozi  mwaka huu baada ya  yeye na mkewe Marya Prudence kumpiteza binti yao  mapema mwaka huu . Baada ya janga ,husemwa muda huwezi kukuba afueni lakini hili huenda likachukua mda mrefu kwa familia hii change .

https://twitter.com/WillisRaburu/status/1220218139885146112?s=20

Ameingia katika twitter Raburu ,ili kujaribu kueleza tu jinsi kumpoteza mtoto wao kumemnyima  ‘mwanga’ maisha na ameandika (Imetafsiriwa)

‘ Maisha yangu yalipoteza mwanga ….wakati rangi yangu ya kung’aa zaidi ilipochukuliwa…. Sasa najaribu tena kujikamua…safari inaendela’.

 Ujumbe wak huo umetoa taswira ya jinsi ilivyo kibarua kigumu kwa mzazi au mtu kukubali kumpotezwa mpendwa wake . kwa bahati nzuri mashabiki wake wengi wamempa moyo na kumtumia jumbe za kumtaka awe na matumaini ya kuweza kuuata ‘mwanga’ mwingine katika maisha yake .Raburu  na Marya  walifunga ndoa mwaka wa 2017 katika hafla ya kibinafsi iliyohudhuria na jamaa na rafiki zao wa karibu.