Sijafanya lolote baya:Ajitokeza kusema Gladys Shollei baada ya picha na mzungu kusambaa mtandaoni

Shollei
Shollei
Mwakilishi wa akina mama Uasin Gishu  Gladys Boss Shollei amekanusha ukiukaji wowote wa maadili baada ya kusambaa kwa picha zinazomwonyesha akiwa pamoja na mwanamme mwingine  ,mzungu siku chache tu baada ya kutalakiana na mumewe  Sam Shollei .

Bi. Shollei alifanya kikao na wanahabari mjini Eldoret kwa muda wa dakika tano  na hakukubali kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari . Amesema kamwe hatojibu maswali kuzihusu picha hizo  au madai dhidi yake .  ameongeza kwamba maajuzi ametishiwa  kwamba jina lake litaharibiwa na anasema tukio hilo la kuzichaoisha picha hizo katika mitandao ya kijamii ni sehemu ya  hila hizo dhidi yake .

Shollei amesema hakuna kampeini ya kumharibia jina  itamzuia kuwahudumia wakaazi wa Uasin Gishu  na taifa . Ameongeza kwamba licha ya picha hizo kusambazwa mtandaoni ameendelea kufanya kazi yake bila usumbufu wowote  na hata alikuwa katika mahojiano ya runinga akizungumzia masuala yanayowaathiri wananchi wa eneo lake .

Shollei amesema changamoto zinazomkumba kwa sasa sio za kwanza na  hazitadumu huku akishikilia kwamba ataendelea na majukumu yake ya kuwatunza watoto wake na kuwafanyia kazi wapiga kura .