Msinitishe:Rais Kenyatta asema hatotikiswa na yeyote katika kuwaunganisha wakenya .

Uhuru kenyatta
Uhuru kenyatta
  Rais Uhuru Kenyatta amekariri kujitolea kwake katika kuliunganisha taifa . Amesema juhudi zake zitamaliza ghasia za kila mara ambazo hushuhudiwa kila wakati wa uchaguzi mkuu ."Nchi ikiwa na amani na umoja mengi yanaweza kutendeka, sio kila saa ni siasa. Nawaomba wenzangu muambie wanasiasa wacheni tufanye kazi kwanza," Uhuru  amesema.

Rais ameyasema hayo siku ya jumanne  katika eneo la Salgaa,Nakuru  wakati wa kufunguliwa kwa kiwanda cha kitaifa cha saruji .  Amesema juhudi zake zinalenga kuhakikisha kwamba wakenya wanasalia na umoja na kusonga mbele  pamoja .

"Tusiogope tukiwa pamoja. Ndio kitu muhimu kwa nchi hii ili iweze kusonga mbele. Na mimi sitatingizika.Hapo ndipo mimi nipo na nitasonga mbele na hiyo line,"   Rais amesema . Kenyatta amesema kiwanda hicho cha saruji  kitachangia kuafikia malengo ya ajenda zake kuu nne kwa kuwapa wakenya ajira . Amesema serikali itazidi kushughulikia changamoto  zinazowakabiliwa watengezaji bidhaa .