Alinilazimisha kusafisha maiti kahaba wa Mombasa akiri

prostitutes_421217179-696x351
prostitutes_421217179-696x351
Kazi ya ukahaba imeendelea kukolea na kukiti mizizi nchini kwa sababu bainifu na wengin wanapoulizwa wanasema wamekosa ajira ,kejeli kutoka kwa familia zao na kutaka pesa za kujikikmu na kadhalika.

Inawalazimu  baadhi yao kuungilia kazi hizo licha ya hatari na changamoto zinazowakodolea macho wengi wao waliozamia tendo hilo.

Yamkini "Wafanyabiashara"hao hawakai nyumbani tu wakingoja mteja wao bali helekea katika maeneo ya kujivinjari kama vile klabu,bara barani,na hata mitaani nyakati za usiku kubahatisha iwapo watapa mteja.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na mmoja wao,Jane,ambalo si jina lake anasema alipopatana na mteja kwa mara ya kwanza na kumpa shilingi 5000 alifurahia sana japo hakuwa na ufahamu kuwa tulikuwepo na kazi nyingine ambayo alistahili kuifanya kando na ile anayoifanya.

"Tulienda nyumbani mwake Nyali badala ya kufanya ngono, alinitolea maiti alioniambia ni ya mke wake,

Aliniambia nisafishe kwa sababu uwa analipa mtu aisafishe na kuirembesha."Alieleza Jane.

Jane mama wa watoto wawili anasema anafanya kazi hiyo ili kuwakimu wanawe aghalabu waweze kupata chakula cha kila siku na mahitaji mengine.

Vile vilev anasema panapandashuka katika biashara hiyo ikiwemo kutishiwa kuuwawa na wateja wengine,mfano alishikiwa bunduki na mteja wake baada ya kudinda kusafisha mwili wa maiti.

"Nilipokataa kusafisha mwili alinichapa na kisha kuchukua bunduki na kunionyesha, na kudai sifahi kukataa kwa sababu alikua ashaanilipa." Aliendelea kueleza.

Kando na kuenzi kazi hiyo maisha yao yamo hatarini kwani hawafahamu ni mteja yupi watakutana naye na hali yake ya afya iko  namna gani.