Ataponea? Mo Farah atuhumiwa upya na swala la madawa ya kusisimua misuli

Maswali mapya yameibuka juu ya uhusiano baina ya Mo Farah na kocha wake wa zamani Alberto Salazar yaliyojitokeza katika uchunguzi mpya wa kipindi cha BBC Panorama.

Nyaraka zinaonyesha kuwa farah alikanusha mara kwa mara kuwa alidungwa sindano za madawa ya kututumua misuli michezoni ya L-carnitine kabla ya mbio za London Marathon 2014, alipoulizwa na wachunguzi wa shirika la Marekani la kupambana na madawa hayo (Usada).

Farah baadae alibadili maelezo yake kwa wahunguzi wa Usada, akisema kuwa alikua amesahau.

Nyaraka pia zilifichua jinsi maafisa wa riadha wa Uingereza walivyopelekwa nchini Uswisi kukusanya madawa yanayokubalika kisheria kutoka kwa mtu aliyefahamiana na Salazar.

Baruapepe ambazo Panorama ilizipata zinaonyesha ni jinsi gani maafisa wa riadha wa Uingereza walivyoelezea awali hofu yao juu ya ikiwa sindano hiyo ilikua salama ''kimichezo''

Kipindi cha Panorama ' Sakata ya Mo Farah na Salazar' itaangaliwa Jumatatu , 24 Februari.

Salazar anaendesha mradi wa Nike Oregon - ambako kumekuwa nyumbani kwa mshindi wa marambili wa Olypmpiki Farah kuanzia 2011 hadi 2017.

Mwaka 2015 uchunguzi wa Panorama kwaushirikiano na wavuti wa Mrekani ProPublica, mara ya kwanza ulifichua madai ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli michezoni ya Salazar, kocha ambaye alisifiwa kwa kiasi kikubwa kwa kumsaidia Farah kuwa mwanariadha bora zaidi Muingereza.

Kipindi kiliibua uchunguzi wa Usada , uliosababisha Salazar kuwekea marufuku ya miaka minne ya kutoshiriki micheo na mahakama ya mizozo ya kimochezo nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka 2019.

Salazar anakana matokeo ya uchunguzi na amekata rufaa dhidi ya marufuku iliyowekwa dhidi yake.

Katika taarifa yake alisema kuwa : "Jopo lilisema kwamba nilifanya kwa 'nia njema' na bila 'nia mbaya ya kukiuka sheria na maadili '.

Sheria mbili zilizokiukwa na Salazar zinahusiana na matumizi ya njia zilizopigwa marufuku ya za kuchomwa dawa ya L-carnitine, ambayo ni dwa inayokubalika kisheria.

L-carnitine ni kichocheo halisi halisi kisicho na madhara ambacho hubadilika na kuwa amino acid, ambayo, mtu akichomwa inakwenda moja kwa moja katika mishipa ya damu, baadhi ya watafiti wanasema kinaweza kuharakisha kuongeza nguvu za mwili na kuinua ubora wa mwnariadha kimchezo.

Matumizi ya kichocheo hicho yaliruhusiwa miongoni mwa sheria za Shirika la kupambana matumizi ya madawa ya kututumua misuli michezoni duniani (Wada) ambapo kiwango kilichokubalika ni chini ya mililita 50 kila baada ya saa sita.

Mwaka 2014, Farah alimaliza mbio akiwa wa nane katika mbio zake za kwanza za london Marathon.

Soma mengi