Yuko wapi Gavana Cyprian Awiti ?

Awiti
Awiti
NA NICKSON TOSI

Ni karne ya Ishirini na moja ambapo mataifa mengi yamepiga hatua katika uimarishaji wa miundo msingi kama kuimarisha sekta ya afya ,elimu,bara bara na kilimo.

Ni wapi taifa la kenya lilikosea,ni wapi tulikosea miaka saba baada ya kuanzisha ugatuzi nchini,na ni wapi wananchi wa kenya walikosea walipowachagua viongozi ili kufanikisha kuwa mahitaji yao yanaafikiwa?.

Wakaazi wa kaunti ya Homa Bay hawana cha kufurahia kuhusiana na ugatuzi baada ya picha za hospitali kuu ya kaunti hiyo kuzagaa mitandaoni zikionyesha wagonjwa waliolazwa hospitalini wakiwa wamelala kwa vitanda bure bila blanketi.

Matunda ya ugatuzi ni yapi?,

Hattua za haraka ni sharti zichukuliwe na uongozi wa rais Uhuru Kenyatta ili kuhakikisha kuwa vviongozi wazembe kama Cyprian Awiti hawakai katika afisi za umma wakiendelea kupokea mishahara mikubwa mikubwa bali kazi wanayofanya ni tuni na hairidhishi hata kidogo.

Iwapo rais Uhuru Kenyatta anataka ajenda moja wapo kati ya nne kuu ya afya bora kwa wote inataka kuafikiwa ni sharti hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo kusimamisha pesa zozote zinazotumwa kwa kaunti kwa minajili ya maendeleo.

Je,ni vipi pesa zinazotumwa na serikali kuu kwenda katika kaunti ya Homa Bay hutumiwa na uongozi wa Awiti?

Wabunge ,Seneta na muakilishi wa kaunti ya Homa Bay walipotelea wapi kuona uozo uliokolea katika kaunti ya Homa Bay.

Ni maswali tu ambayo yanaweza jibiwa iwapo asasi zote husika zitaamka kutoka kwa lepe la usingizi na kuakikisha kuwa viongozi kama Cyprian Awiti wanag'atuliwa kutoka kwa mamlaka .

Serikali za kaunti zimekuwa kipaumbele kuwatoza wananchi wakev ushuru kila siku ,kwa kile magavana wanataja kuwa ni kufanikisha maendeleo katika magatuzi hayo.

Je?,Magavana kama Cyprian Awiti wanastahili kuhudumu katika afisi za umma hata baada ya rekodi mbaya ya maendeleo.