‘Ilikuwa jokes na akaniacha hivyo tu’ Mchezo wa kubana ngono wasababisha machozi

Woman
Woman
Kuna  michezo ya kiutano ambayo wapendana o hupenda kushiriki ili kupoteza muda na au hata  kujivinjari.

Lakini mchezo alioanzisha  Benta   kwa mpenzi wake Jotham ulikatiza uhusiano wao mara moja ,na  Ulikuwa ni utani tu ! Benta na Jotham walifanya bet ili kuona ni yupi kati yao hangeweza kukaa  kwa muda wa miezi miwili bila kuitisha ngono . Benta  anasema  mchezo huyo wa kamari ulifaa kuwa utani tu kumbe Jotham aliuchukulia kwa  uzito na pia akafikiri iikuwa njama ya mwenzake kukataa kushiriki mapenzi naye .Bila kufahamu kwamba  Jotham alichukulia jambo hilo kwa ubaya Benta aliendelea kubana ngono asiweze kuitisha tendo la ndoa kutoka kwa mpenzi wake.Baaada ya wiki moja bila mmoja wao kuitisha haki hiyo ,Benta aligundua kwamba mpenzi wake alikuwa ameanza kununa .

Muda mfupi baadaye alianza kulala mapema na kuangalia upande wa ukuta asitake hata kusumbuliwa . Ikamjia fikra kwamba labda huenda alikuwa amepata mpenzi wa pembeneni aliyekuwa akimtosheleza . Benta alipata na mshangao alipomuuliza Jotham kuhusu tabia yake kwani alimkumbuisha kuhusu ‘bet’ walioweka ili kuona ni yupi atastahimili miezi miwili bila kuitisha ngono kutoka kwa mwenzake .

Waliosema  mzaha mzaha hutumbukia usaha   walijua walicholenga kusema kwani baada ya mwezi mmoja bila wawili hao kujamiana kama wapenzi ,  Jotham alimtumia  Benta ujumbe wa simu akimuambia kwamba hataki tena kuwa katika uhusiano naye .Benta alishangaa sijue amemkosoa nini mwenzake na jaribio lake  la kutaka kujua sababu za yeye kukatiza uhusiano wao  halikufaulu .

Baadaye aligundua kwamba Jotham alikuwa karudiana na mpenzi wake wa zamani! Sababu? Kwamba Benta alikuwa hataki kumpa tendo la ndoa na hivyo basi akaanzisha  ule mchezo wa kutoitisha ‘tunda’ kutoka kwa mwenzake. Benta anasema anajutia mchez ule lakini chao wote wawili ndicho anasema kilisababisha uhusiano wao kukatika  kwa sababu hakuna kati yao aliyekuwa tayari kushusha moyo ili kuzungumzia suala hilo . Uhusiano wao wa miaka miwili ulikatika hivyo kwa sababu ya mzaha.