Uhuru amuomboleza Chief Inspector wa polisi Pius Kipserem

Uhuru kenyatta
Uhuru kenyatta
Rais uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa kuifariji familia,jamaa na rafiki za  Chief Inspector  wa  Police Pius Kipserem Cheboswony.

Cheboswony,  aliyega dunia jumatatu katika ajali ya barabarani  kwenye barabara ya  Oljororok-Dundori Road huko nyandarua alikuwa akismamamia Ikulu ndogo ya Sagana ana alikuwa amehudumu katika huduma ya polisi kwa miaka 28 .Katika ujumbe wake rais amesema taifa limempoteza  afisa wa usalama aliyekuwa wa kujituma  na ambaye kujitolea kwake kulimfanya kupendwa na wenzake.

Rais amesema ameiombea familia ya marehemu ili wapate kufarijika baada ya msiba huo .