Sina ufahamu iwapo mashabiki wangu wanadai mimi ni mkali kuliko Diamond! asema Harmonmize

hamon.jfif
hamon.jfif

NA NICKSON TOSI

Msanii wa nyimbo za kizazi kipya ukanda huu wa Afika mashariki na kati Harmonize amekuwa akitia fora sana katika utendakazi wake haswa baada ya kutoa albamu yake mpya  ya nyimbo 18 akiwashirikisha wasanii wengi na maarufu wakiweno,Burna Boy,Yemi Alade,Marioo na Khaligraph Jones na wengine wengi.

Siku za hivi karibuni tumekuwepo na gumzo mitandaoni haswa baada ya Harmonize kung''atuka kutoka lebo ya WCB na kuibua gumzo miongoni mwa mashabiki kuhusiana na ni nani mkali kati yake na Diamond.

Mmoja wa shabiki wa Harmonize katika mitandao yake kwa jina H-Baba ndiye amekuwa akieneza jumbe za kutaka mashabiki kufanya uamuzi wao kubaini nani kati ya wasanii hao wawili ni mkali kuliko mewengine,lakini alipokuwa katika mahojiano na stesheni moja ya Tanzania,Harmonize alimtaja H- Baba kuwa rafiki nma shabiki wa karibu nma kile anavchoandioka katika mitanmdao yake ya kijamii hawezi fahamu hata.

''H. Baba ni moja ya Kaka zangu kama walivyo wengine ila anachokifanya mitandaoni mimi siwezi kumpangia" alisema Harmonize.

Matamshi ya Harmonize yanajiri siku chache tu baada ya H- baba kutuma ujumbe wa kumdhihaki Diamond katika ukurasa swake wa instagram akidaio kuwa haikustahili Diamond kumshurutisha Harmonize kulipa dhamana hata baada ya kuhitimisha mkataba na kampuni ya Diamond.

H- baba alisema kuwa ingekuwa vhyema kama Diamonmd alikuwa anamguza kitalanta Harmonixze kumruhusu kutoka katika lebo yake bila kulipa chochote iwapo alikuwa anapania kumsaidia katika maisha yakle.

Mwaka jana ,Harmonize alilazimishwa kulipa shilingi milioni 22.4[Tsh500Milioni],hela zilikuwa zinamruhusu kukatisha mkataba wake baina hyake na kammpuni ya WCB na wakati huo kumwezesha kuwa mmiliki wa nyimbo alizokuwa ametoa na lebo hiyo.

Wikendi Harmonize alifungua kinywa kwa mara ya kwanza na kudai kuwa alilazimika kulipoa hela hizo xzote ili kumwezesha kuwa huru baada ya kuwa chini ya umiliki wa lebo ya WCB.

Alidai hayo alipokuwa anazindua albamu hyake mpya ya AfroEast ,uzinduzi ambao ulihudhuriwa na rais wa kitambo wa Tanzania Jakaya Kikwete .

"Kwa sasa tuseme tu nimekamilisha kile kiasi cha pesa ambacho nilikuwa nilepe. Lakini nitasema busara nyingi sana ilitumika kwa pande zote kufikia mwafaka ule"'

 "Nilitakiwa kulipa million 500, Kiukweli kule sijaondoka kwa ubaya, tumefuata sheria na taratibu za mkataba! Nilitakiwa kulipa million 500 na baadhi ya gharama, kiukweli sikuwa na pesa lakini nimeuza baadhi ya mali zangu ili nifanikiwe kulipa hiyo pesa na kwa asilimia kubwa nimelipa bado asilimia chache tu ili niweze kutumia kitu chochote kinachomuhusu Harmonize".alisema Harmonize.