Maafisa wa polisi wachukuwa usimamizi wa feri baada ya tangazo la rais Kenyatta

NA NICKSON TOSI

Uongozi wa feri nchini umechukuliwa rasmi  na maafisa wa polisi na baadhi ya wafanyikazi wa serikali baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa tangaza la serikali kuchukuwa udhabiti wa feri nchini na kuangazia shughuli zote za feri.

Yamkini watu zaidi ya 300,000 hutumia kivukio cha Likoni kila siku na magari takriban 6000 yanayotumia kivukio hicho pia.

Uhuru alitokeza kuwa maagizo yatakayokuwa yanatolewa na maafisa hao ni sharti yazingatiwe.

Katika kivukio hicho cha Likoni imekuwa vigumu kwa serikali kudhibiti idadi kubwa ya watu haswa wakati huu taifa la Kenya limekumbwa na visa vingi vya Corona.

Yanajiri haya saa chache tu baada ya meneja msimamizi wa halmashauri ya bandari nchini Daniel Manduku kujiuzulu kufuatia madai ya ufisadi na utoaji zabuni usiozingatia sheria, madai yaliyompelekea yeye kushikwa .