Leta hii jamaa hapa! Makachero kutoka DCI wamsubiri naibu gavana wa Kilifi

kilifi
kilifi
NA NICKSON TOSI

Makachero kutoka afisi kuu ya mpelelezi mkuu wa serikali DCI wamekita kambi  katika hospitali kuu ya kaunti ya Mombasa wakitarajia kumtia pingu naibu gavana wa gatuzi la Kilifi Gideon Saburi.

Yamkini Saburi ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu wiki chacha kwa kuwa chini ya uangalizi na madaktari baada ya kupatikana na virusi vya Corona.

Hiyo jana waziri wa afya Mutahi Kagwe alidhibitisha kuwa Saburi atafunguliwa mashtaka baada ya kukataa kujitenga siku chache tu baada ya kurejea nchini kutoka Ujerumani ,amri hiyo ilitolewa na serikali lakini Saburi hakutii amri hiyo.

Kwa sasa taifa la Kenya ni watu 110 na ambao wameathirika na Corona huku watu 4 wakiwa wamepona na kuruhusiwa kuenda nyumbani.