Kenya yapokea msaada wa millioni 320 kutoka Denmark kupigana na virusi vya corona

EUp3Wq-XgAAtIqM
EUp3Wq-XgAAtIqM
Baada ya Kenya kuthibitisha visa zaidi ya mia moja na kurekodi vifo vinne na watu waliopona wanne, Jumapili Denmark imetoa msaada wa shilingi  millioni 320.

Waziri wa maendeleo nchini Denmark Rasmus Prehn alisema kuwa pesa hizo zitawekwa katika benki ya Kenya kushugulikia  mahitaji ya  kupambana na ugonjwa wa covid-19.

Ripoti ya balozi wa Kenya ilisema pesa hizo zitatumiwa kununua bidhaa za matibabu na ujenzi wa vyumba vya kuweka wagonjwa hao na hata kutumiwa kwa gharama ya wagonjwa.

The spread of coronavirus seems inevitable...if not handled resolutely, it will have fatal consequences for the most vulnerable populations, not least in densely populated areas and where the health system is challenged ." Prehn Alizunguumza.

Kwa sasa, nchi ya Denmark imethibitisha visa 3672 vya virusi vya corona na watu 139 kuaga  dunia kwa ajili ya virusi hivyo

Awali benki ya dunia ilitoa msaada wa billioni 6 ili kusaidia  Kenya kupigana na virusi vya corona, huku rais akipunguza mishahara ya mawaziri, wake na naibu wake kwa asilimia tofauti ili kusaidia nchi kupigana na virusi hivyo.

Benki kuu ya Kenya  ilitoa msaada wa billioni 7.4 ili kupigana na virusi vya corona.