Kutana na Slayqueen mwanasiasa ambaye anatesa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii

88279164_771077013711180_638240634916848464_n
88279164_771077013711180_638240634916848464_n
NA NICKSON TOSI

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kirinyaga Wangui Ngirici amekuwa kwenhye gumzo haswa katika mitandao yua kijamii baada ya kuonekana akinengua kiuno kwenye shindano la Don’t rush Social Media Challenge.

Shindano hilo linajumuisha washindani ambao hurekodi video yao wakitoka kwa kitanda na kuonyesha brashi ya kujipodoa kwenye kamera ,ambayo sasa huwaonyesha wakiwa wamebadilika kimavazi na hata kisura .

Kwenye video yake ,Ngirici anajirekodi mwanzo baada ya kuamka bila vipodozi vyovyote na nywele zake zikiwa zimefungwa vizuri.

Baada ya kuchukuwa brashi yake na kuonyesha kwenhye kamera ,picha zake zinawadia zikionyesha jinsi alivyobadilika na kuashiria urembo wake halisi.

Mwakilishi huyo baada ye anaonekana akiondoka kwenye gari lake baada ya shindano lake.

Tazama video yenyewe hapa

 Milicent Omanga pia amejipata katika mchezo baada ya kuweka video yake kwenye mtandao wa Twiter