'Alifungiwa Murang’a na lockdown ya Nairobi, i'm so happy!’ Mwanamke aeleza furaha yake

Utataraji  wanaopendana kusononeka endapo watatengana kwa hata  siku moja lakini muda huu wa coronavirus umefungua  mengi tu kuhusu ndoa za watu wengi .

Utahisi vipi iwapo utagundua kwamba mumeo au mkeo amefurahi kwamba huwezi kurejea nyumbani kuwa naye? Basi hayo ndio masaibu ya mwanamme mmoja  ambaye alienda nyumbani katika kaunti ya Murang’a  na akiwa huko , rais Uhuru Kenyatta akatangaza marufuku ya watu kuingia Nairobi .  Ungetaraji kwamba mke wake  angefadhaishwa na habari hizo lakini Mama  Angel  amefurahi kupindukia kwamba mume wake hawezi kuingia jijini kwa siku 21 zijazo ! Kisa na maana...

‘ Haki alikuwa amenichosha! Kila wakati mume wangu akipata fursa haniachii muda wa kupumzika , anataka tendo la ndoa. Mchana kutwa nafanya kazi zote za kufua nguo, kuosha vyombo na hata kupika, mwili umechoka lakini inapofika usiku, tena naanza kibarua cha kumtosheleza mtu!’  Mama Angel anasema.

Mume wa mtu alipojaribu kuwasiliana na mke wake kuhusu uwezekano wa kutumia njia za panya root hadi Nairobi , mke wake alimshaiwishi asifanye hivyo, sio kwa sababu ya kutii amri ya serikali, bali amechoka naye na amefurahia mapumziko anayopata kwa  sababu mume  yuko mbali .

‘ Aliponiambia eti anakuja kupitia njia za vichochoroni, nilimtishia nikamuambia akipatikana atapelekwa quarantine-Kusikia hivyo, kamekubali kubaki Murang’a hadi  lockdown ya Nairobi iishe’  Mwanamke huyo anasema akicheka .

Kuhusu iwapo alikuwa amechoka na mumewe hata kabla ya janga la virusi vya Corona kuja, mwanamke huyo anasema  hali haikuwa hivyo kwa sababu mumewe alikuwa akienda kazi na wangefanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki .

‘Kwa sababu haendi kazi siku zote hizi, amekuwa akiamka akifikiria tu kuhusu tendo la ndoa , mchana, usiku na hata  anaambia watoto wacheze nje ndio apate fursa ya kunirukia’.  Anasema  mama Angel.

Serikali maajuzi imetangaza mikakati ya kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona kwa kupiga marufuku usafiri wa watu kuingia na kutoka Nairobi, kaunti za Kwale, Kilifi na Mombasa. Mamia ya watu waliokuwa wakitoka au kuingia katika maeneo hayo walitatizika sana  lakini serikali imeeleza kwamba hatua hiyo sio ya kuwatesa bali ya kuwalinda.