Haya hapa mambo ambayo huyajui kuhusu msanii mpya wa WCB Zuchu Kopa

Diamond Platnumz amemsaini msanii wa kike katika lebo yake ya muziki miaka minne baada ya dada yake Queen Darleen kuondoka katika lebo hiyo.

Zuchu tayari ameshatoa wimbo ambao umependwa na wengi ambao unafahamika kama ‘wana’

Kupitia mtandao wa kijamii, alisema kuwa hatawahi kuangusha mashabiki wake. Hii ni baada ya Diamond kufichua siri hiyo.

"NASHUKURU BIG BOSS 💙❤️NAHAKIKISHA SITO KUANGUSHA KATIKA SAFARI YANGU HII MPYA YA MZIKI 🙏🙏 WCB FOREVER." Aliandika uchu.

Haya hapa mambo ambayo huyafahamu kumhusu Zuchu.

1.Zuchu ni maneja wa mama yake Khadija Kopa. Huwa anamsaidia sana katika kazi yake

2.Kama vile mama yake anafahamika sana, Zuchu awali aliimba wimbo wake na msanii Diamond unaofahamika kama ‘nasema nawe

3. Katika familia yao ina watoto wanne, ndugu yake Omar Kopa aliaga dunia akiwa na miaka, 23, baada ya kuugua kwa muda.

4.Ni mwanawe msanii wa taarab wa nchi ya Tanzania ambaye anafahamika sana Khadija Kopa ambaye alianza usanii wake mwaka wa 1990.

Je Zuchu ataweza kutoa vibao motomoto baada ya kuwa miongoni mwa wasanii wa WCB? Tunamtakia kila lakheri kwa safari hii yake.