Ni kubaya! Hakuna kubeba watu 3 katika gari la kibinafsi

roadblock
roadblock
Unajitia katika hatari ya   kukamatwa na kufungwa jela kwa miezi sita au kutozwa faini ya shilingi 20,000 endapo  utapatikana ukisafiri na  zaidi ya watu watatu katika gari la kibinafsi.

Iwapo unatumia teksi basi hakikisha kwamba ni wewe  na dreva wa teksi pekee yenu .

Dhamira ni kuzuia usambaaji wa virusi vya corona. Serikali imepiga marufuku usafiri wa zaidi ya watu watatu katika  gari la kuwabeba watu watano. Gari la kuwabeba watu 7 sasa litawabeba watu watatu  akiwemo dereva .

Hatua hizo kali ni miongoni kwa zilizotangazwa na waziri wa  Afya  Mutahi Kagwe  na kuwekwa katika  gazeti  rasmi la serikali  ili kuzuia kusambaa virusi  vya corona

Msemaji wa serikali  Cyrus Oguna  amesema kwamba arifa hiyo ya gazeti rasmi la serikali sasa ni sharia na polisi wanafaa kuwakamatwa  wanaokiuka  agizo hilo. Msemaji wa polisi  Charles Owino amesema amesema maafisa wa huduma ya kitaifa ya polisi wanafaa   kuanza kutekeleza  sheria hiyo mara moja .