Juzi ilikuwa Zari!' Ringtone 'mashakani' baada ya kuonekana na Tanasha

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko, amejipata taabani, mikononi mwa wakenya baada ya kuchapisha picha yake na mrembo Tanasha Donna.

Licha yake kuandika 'A man of God meating a woman of God who is very polite with pure heart' hilo halikuwazuia wakenya ambao ni dhahiri kuwa hawajasahau vishasha vyake vya hapo awali.

Hapo awali Ringtone alishangaza wengi alipomnunulia aliyekuwa mpenzi wa Diamond, Zari Hassan gari la aina ya Range Rover, kama zawadi iwpo atampa fursa ya kuwa katika uhusiano naye.

Isitoshe, Ringtone alionesha picha ya mifugo atakaotumia kulipa kama mahari yake Zari ila hakufua dafu.

Alipoulizwa kama anamtambua Ringtone, Zari alisema hamjui na kamwe hajwahi kutana naye.

"I don't know Ringtone and I have never met him. This is actually news to me. I have over 3.9 million followers on Instagram and I wouldn't know who follows me," Alisema Zari.

Kile ambacho wengi waliuliza ni je, mbona yeye hungoja Diamond awateme wapenzi wake kabla yae kuonekana nao?

Soma baadhi ya ujumbe kutoka wakenya;

Mulamwah: Bro ilikua Zari, umechange tena mondi ndio pacesetter naona

Sharon: Si Zari tena

Nickie: Si unapenda burungu zimeachwa na latnumz, si zari ndo huyu tanash..naenda ivi nakam

eatweel: Unapenda leftovers za Diamond

Valmesut: Unapenda maex wa Diamond

rastone: Ayee bado unamtafuta diamond maneno