Hatimaye, Nandy apata mwanamume wa kumlipua 'lungula' ya kutosha

pjimage (34) (1)
pjimage (34) (1)
NA NICKSON TOSI

Kwa miezi sasa msanii kutokea Tanzania Nandy amekuwa akihusishwa na wanaume kadhaa wanaosemekana walikuwa wanamchumbia lakini kichuna huyo huenda amepata mwanamume wa kulimpua lungula ya kutosha baada ya kuwa kwenye kibaridi kwa muda sasa .

Katika video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ,Nandy ameamua kutulia  na jamaa kwa jina Bill Nas ambaye kwa muda sasa wamekuwa wakionekana na Nandy pamoja japo swala la kuhusiana na iwapo walikuwa wanachumbia hawakuwa wameliweka wazi.

Bill Nas alionekana akimvisha Nanndy pete jugwaani mbele ya umma.

Kisa hicho kilitokea pale Nandy alipokuwa anawatumbuiza mashabiki wake na kisa Bill kutokea ghafla akiwa na kumkumbusha kule ambako wametoka na wawili hao kwa mapenzi yao.

Tumekuwa pamoja kwa muda sasa na tumepitia changamoto si hapa,kutoka kwa mazuri na mabaya ,nafahamu uzuri wako na pia ulegevu wako.Nataka ulimwengu mzima leo kufahamu kuwa mimi Bill Nas nakupenda na nitaendelea kukupenda ,alisema Bill Nas.

Nandy alitokwa na machozu baada ya kuvalishwa petre hiyo na Bill na kisha kumpa busu kama njia ya kumdhihirishia Bill kuwa yeye pia alikuwa ashampenda.

Wawili hao walikuwa wamewahi kuchumbiana miaka ya pale nyuma kabla ya kuachana na Nandy kuanza urafiki na Ruge ambaye aliaga kabla ya kufungu fungate.

Uvumi ulikuwepo kuwa labda Nandy alikuwa anachumbiana na Willy Paul swala ambalo kwa sasa ni kama limezikwa kwenyer kaburi la sahau.