Baada ya Nyashinski kutoa albamu yake,macho yote sasa yaangazia Sauti Sol

NA NICKSON TOSI

Washindi wa tuzo ya Afro Pop Sauti Sol wanatarajia kuzindua albamu yao ya 5 ya  Midnight Train tarehe 5 Juni mwaka huu ikiwa ndiyo albamu yao ya kwanza kufanya chini ya lebo ya Univrersal Music Africa.

Kupitia kwa mtandao wao wa Instagram Sauti Sol walisema watazindua kanda hiyo ambayo itakuwa na nyimbo kama Suzzana mnamo juni 5.

Our 5th studio album drops June 5th.waliandika Sauti Sol

Katika albamu hiyo kutakuwepo na wasanii kama vile India Arie katika wimbo wa My Everything , na msanii Burna Boy katika wimbo wa Time flies.

Albamu ya Midnight Train itakuwa na nyimbo zifuatazo tazama.

  • Intro
  • Midnight Train
  • Insecure
  • Feel My Love
  • Brighter Days ft. Soweto Gospel Choir
  • Nenda Lote
  • Suzanna
  • Interlude
  • My Everything ft. India Arie
  • Wake Up ft. Mortimer
  • Sober
  • Time Flies ft. Burna Boy
  • Disco Matanga (Yambakhana) ft. Black Motion & Sho Madjozi
  • Rhumba Japani ft. Kaskazini, Bensoul, Xenia, Nviiri, Okello Max, NHP

Uzinduzi wa albamu ya Sauti Sol utajiri baada ya msanii mwengine kutokea humu nchini Nyashinski kuzindua albamu yake LUCKY YOU