Mna ujinga sana! Mnaeneza jumbe za unajisi kwa nini? Wakenya wakasirishwa na wimbo mpya wa Ethics

Ethic-1
Ethic-1
NA NICKSON TOSI

Kwa mara nyingine tena, wanamuziki wa kikundi cha Ethics nchini wamejikuta katika  njia panda baada ya kutoa wimbo unaeneza jumbe za kufanya kitendo cha  ubakaji nchini kuonekana kama kitu halali.

Kinaya ni kwamba, licha ya kukashifiwa na wakenya wengi, Ethics kwa mara hii wamefanya wimbo kwa jina Soko ambao baadhi ya maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanaeneza ujumbe kuwa kitendo cha kunajisiwa si kinyume cha sheria  hali ambayo imewakasirisha mamia ya wakenya.

Wololo! Zambian MPs visit Kenya to learn how to fight corruption

Miongoni mwa wale waliokasirishwa na kitendo hicho ni  Tedd Josiaha ambaye amesema vijana hao wanatafuta umaarufu kwa kutumia mbinu za kitambo zisizo na maadili yoyote.

Tedd amesema kuwa nyimbo kama hizo zinaangamiza sanaa ya muziki wa Kenya kwani maneno yaliyotumika hayawezi kufanya wasanii wengine nchini kutoa nyimbo ambazo zinaweza kuendeleza sanaa hiyo.

Ujumbe wa Tedd Josiah alioandika kuhusiana na wimbo huo ni huu hapa tumeunakili kwa lugha ya kiingereza.

Rape culture is a huge NO! You 2-bit silly Gengetone artistes and producers I want u to sit ur punk asses down right now and listen! You’re killing an industry called the music industry of Kenya when it’s already on its knees! Why y’all wanna start talking bout raping little infants 👶🏽 in your tracks? Why y’all wanna make ladies our beautiful Kenyan ladies think that sex is a man’s right and if u don’t give it then u ain’t nothing? Why y’all messing things up for yourselves and all those talented kids trying to come up without stupid music or scandalous stories! Use ur talent not scandals, sex, drugs and all that nonsense you can do much better! Big brother is watching u 👁”aliandika  Tedd

Baadhi ya wasanii wengine kutoka kwa kikundi cha Sailors Peter Miracle Boy pia yeye alikasirishwa na hatua ya Ethics na kuandika hivi.

Siwezi kimya mumechoma😳Rape haifai ku glorifiwa. SHAME ON YOU 🙄 

Mamlaka ya kuratibu ubora wa miziki nchini KFCB haikubaki nyuma bali ilihakikisha kuwa wimbo huo unatolewa katika mitandao yote ya kijamii na kuwatumia wasanii hao onyo kali.

Pandana and Tarimbo wimbo huu ulipigwa marufuku nchini na KFCB baada ya kufahamika kuwa baadhi ya maneno ambayo yalitumika katika wimbo huo yalikuwa ya kupotosha jamii.