Flight baby: Mwanamke kutoka Nigeria ajifungua mtoto katika ndege ya kumrejesha nyumbani

Mwanamke mmoja amejifungua mtoto akiwa safarini katika ndege kurejeshwa  Nigeria  kutoka  Dubai UAE.

Abike Dabiri-Erewa,  mwenyekiti wa   jamii ya wanigeria walioko nje ya nchi  amesema  Kafayat Amusan  alimzaa mtoto wa kiume dakika 30  baada ya ndege kuondoka  uwanja wa ndege. Ndege hiyo ililazimika kurejea Dubai ili kuhakikisha kwamba mama na mtoto wapo salama .

Amusan na mwanawe wapo katika hali nzuri kiafya  na wamelazwa katika hospitali moja Dubai. Wanatarajiwa kurejea Nigeria pindi cheti za  kuzaliwa cha mtoto huyo  kitakapotolewa  na stakabadhi nyingine za usafiri kutayarishwa. Mwanamke huyo alikuwa katika kundi la kwanza la raia wa Nigeria  waliotolewa UAE kurejeshwa nyumbani kwa sababu ya janga la virusi vya Corona .

Watu 256 waliwasili katika uwanja wa ndege wa   kimataifa wa Murtala Muhammed  jijini Lagos  Jumatano saa moja jioni. Maamlaka za Nigeria zimesema zimefaulu kupata sehemu ambazo raia wake wanaorejea watakapotengwa katika karantini.