No Sex! Ugonjwa wa zinaa ulinizuia kufanya mapenzi na mke wangu kwa mwaka mmoja.’ Jamaa aeleza masaibu yake baada ya kuambukizwa STI

black man
black man
Hakuna kinachotisha kama kuambukizwa maradhi  ya zinaa na hasa iwapo upo katika ndoa na umeutoa ugonjwa huo nje ya ndoa kwa sababu ya tabia yako ya usinzi .

Hivyo ndivyo ulimwengu wa  Sam Kolole ulivyompinduka siku moja wakati tamaa yake ya  kujihusisha na mapenzi ya nje ya ndoa  yalimpofanya kuambukizwa ugonjwa wa  kisonono. Anasema kuteleza kwake kulimfanya kulia kama mtoto  kwani kando na uchungu  wa kupatwa na ugonjwa huo, ilikuwa kibarua kuanza kutafuta matibabu na alianza kujipata na fedheha kumueleza mkewe kwamba wangefaa kutibiwa wote pamoja kwa ajili ya  utovu wa maadili yake.

Baada ya kupimwa na  kupatikana na ugonjwa huo, Sam aliogopa kumuambia mkewe kuhusu kilichofanyika na  hakujua iwapo alikuwa tayari ameshamuambukiza mkewe na ndiposa  akajiamulia kwamba kabla ya kufahamu endapo mkewe pia ana ugonjwa huo, hatofanya mapenzi naye na hakushiriki naye tendo la ndoa kwa mwaka mmoja.

Hapo ndipo matatizo yake yalipoanzia kwani mkewe alianza kushangaa mbona Sam hakuwa akitaka kujamiana naye . Alitafuta vijisababu kila mara wakati mkewe alipotaka washiriki tendo la ndoa na hatimaye kwa sababu ya kuogopa kumueleza kilichokuwa kikifanyika, mkewe aliamua kumuacha na kuondoka .

Baada ya kutibiwa  na kupona, Sam sasa amepata ujasiri wa kumueleza mkewe kilichofanyika na akitaka warudiane  kumbe tayari mkewe alivyokwenda aligundua kwamba alikuwa pia na ugonjwa huo na akatibiwa alikokuwa amekwenda. Amekuwa na hamaki muda wote huo akikosa kuamini kwamba mumewe  alikuwa akishiriki mapenzi hatari nje ya ndoa na hata kuambukizwa ugonjwa wa zinaa. Isitoshe, kando na tabia yake hiyo iliyohatarisha afya zao, aliogopa kumuambia naye pia apimwe ili kubaini ili kugundua iwapo ana ugonjwa huo .

Sam sasa  ameachwa na majuto ya mbona hakumueleza mkewe  wakati alipoambukizwa ugonjwa wa kisonono  kwani hatua hiyo sasa imetishia kuigharimu ndoa yake. Wakati alipokwenda hospitalini kutibiwa, madaktari walisistiza kwamba aje na mwenzake ambaye walishiriki naye mapenzi. Sam hakuweza kuja naye kwa sababu anashuku alipata maradhi hayo kutoka kwa kahaba mmoja alipokuwa Kisumu safarini. Pia hangeweza kuja na mkewe kwa sababu angetakiwa kujibu maswali ambayo hakuwa tayari kutoa.