Kula Ruto, Kura Uhuru! Mutahi Ngunyi amkejeli Murkomen baada ya washirika wa Ruto kupigwa shoka seneti

Kauli mbiu ya watu wa ‘Nyumba ya  Mumbi’ ni rahisi :Kula Ruto, Kura Uhuru.

Hayo ndio yaliyokuwa maneno ya  mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi  Jumatatu muda mfupi tu baada ya  Kipchumba Murkomen kufurushwa kama kiongozi wa walio wengi katika seneti.

https://twitter.com/MutahiNgunyi/status/1259804842970820608

"Kama nilivyosema hapo awali, huwezi  kumnunua mkikuyu, utaweza tu kumkodisha kwa muda.’ Aliandika katika twitter .

"To my friend Murkomen, Pole Sana. I will pray for you. Now you have enough time to dry your greenhorns."

Wakenya wengi walitoa maoni  kuhusu hilo  huku Murkomen mwenyewe akicheka  baada ya Mutahi kumuandikia hayo .

https://twitter.com/LOYDMUTUA/status/1259817889764384771

Murkomen  hapo awali alikuwa ameandika katika twitter kwamba bado yupo thabiti .

https://twitter.com/kipmurkomen/status/1259812121715650560

Badaye  Murkomen aliwahutubia wanahabari na kukashifu marekebisho ya uongozi wa seneti. Alisema maseneta wengi hawakuhudhuria mkutano wa Ikulu ya Nairobi uliodaiwa kutekeleza mageuzi ya uongozi katika seneti. Murkomen amesema ataendelea kupigania demokrasia huku akishangaa mbona rais Uhuru Kenyatta anawaelekezea viongozi wa Jubilee hamaki .

Ikulu ilitangaza kupitia taarifa kwa wanahabari kwamba  seneta  wa west Pkot Samule Poghisio  ndiye kiongozi mpya wa walio wengi katika seneti. Naibu wake Poghisio  atakuwa seneta wa Isiolo  Fatuma Dullo Adan. Seneta wa  Murang'a Irungu Kang'ata  ameichukua nafasi ya  seneta wa Nakuru  Susan Kihika kama kiranja wa chama cha walio wengi katika seneti. Seneta mteule  Farhiya Ali Haji ndiye atakayekuwa naibu wa Kang’ata.