Wakaazi kaunti ya Kilifi waogopa kwenda hospitalini

Wakaazi katika kunti ya Kilifi na wanaotafuta tiba wameagopa kwenda hospitalini kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya corona.

Yanajiri hayo siku cache tu baada ya hafla ya kuwapima wakaazi eneo hilo kuingiwa doa baada ya wahudumu kukosa vifaa kamili vya kuwapima wakaazi virusi vya Corona.

Kulingana na takwimu za sensa, kaunti ya Kilifi ina watu milioni 1.4 na mashine ambazo serikali ilikuwa imetuma kuwafanyia vipimo wakaazi hao vilikuwa na uwezo wa kuwapima watu 300 pekee.

Kwingineko ni kuwa kaunti ya Nakuru inaendelea kuimarisha vituao vyake vya afya kwa kuweka vifaa viunavyohitajika ili kukabiliana na virusi vya corona.

Aidha taarifa za hivi punde ni  mwathiriwa mmoja wa virusi hivyo kwenye kaunti hiyo ya Nakuru anaendelea kupata matibabu na hali yake ya afya i salama.