Kaunti ya yapokea vitanda 100 vya kutenga wagonjwa wa corona - Mkusanyiko wa taarifa

1363129-300x225
1363129-300x225
Kama njia ya kujiandaa kukabiliana na virusi hatari vya Corona nchini, kaunti ya Kiambu hii leo imepokea ufadhili wa vitanda 100 vya kufanikisha kuwatenga waathiriwa wa gonjwa la Corona .

Yakijiri hayo, wafanyakazi watatu wa kaunti ya Kilifi wametiwa mbaroni na maafisa kutoka tume ya kupambana na maadili EACC kwa kukosa kuwasalisha stakabadhi za ununuzi wa vifaa vya kufanikisha upimaji wa wakaazi katika kaunti hiyo.

Shughuli ya kuwafanyia wakaazi uchunguzi ililazimika kusitishwa kwa muda Kilifi baada ya wahudumu kukosa vifaa vya kutosha.

Kwengineko ni kuwa, mwanamme wa miaka 19 amefariki baada ya kupokea kichapo kutoka kwa umma Komarock jijini Nairobi Usiku.

Haijabainika wazi ni nini kilichopelekea yeye kupigwa na umma .

Maafisa wa polisi nao wamewapiga marisasi wezi wanne katika barabara ya Kangundo baada ya lalama kutoka kwa wakaazi.

Bastola mbili zilipatikana wakati huo.