Pigo Brazil,Hospitali zashindwa kuhimili idadi kubwa ya wagonjwa wa corona

brazil-696x392
brazil-696x392
Meya wa mji mkuu wa Brazil  São Paulo,amesema huenda hospitali katika mji huo zikalazimika kufungwa kutokana na idadio kubwa ya wagonjwa wa corona wanaoendelea kuwasilishwa kila mara kutoka maeneo tofauti.Sao Paulo ni miongoni mwa miji mikuu katika taifa la Brazil ambayo yameathirika zaidi na virusi hivyo huku watu 3000 wakiwa wameaga dunia kufikia sasa .

Kufikia Jumamosi Brazil ilikuwa inaongoza kwa idadi ya maambukizi baada ya Uhispania na Italia.

Wizara ya afya katika taifa hilo iliripoti visa vipya vya maambukizi 79387 chini ya saa 24 ,na kufikisha watu 241,000 walioambukizwa virusi hivyo.

Vile vile chini ya saa 24,Brazil imesajili vifa 485 ikiashiria kuwa watu waliofariki kufikia sasa ni 16,118,ikiwa ya taifa la tano ambalo liko na maambukizi mengi yua maambukiz duniani.