Msituletee Moshenee sisi! Tuko nyuma ya rais Kenyatta -Gema waamua

unnamed (25)
unnamed (25)
Viongozi wa jamii ya Agikuyu almaarufu kama GEMA wamesema wanaunga mkono maazimio ya rais Uhuru Kenyatta kuunganisha taifa na hatua ya kuamua kufanya kazi na viongozi wa upinzani nchini.

Kupitia kwa mwenyekiti wake Lawi Imathiu, wamesema wanaunga mkono uamuzi wa rais Kenyatta wa kuliunganisha taifa ili kuwepo na amani na utulivu nchini.

Taarifa yao inajiri saa chache tu wakati ambapo kuna ripoti kuwa serikali inapania kumwidhinisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kwenye serikali.

Inaambatana na taarifa nyingine ambapo viongozi wanamuunga mkono naibu wa rais William Ruto walitimuliwa kutoka kwa nyadhifa zao kwenye seneti.

Kulingana na Imathiu, hatua ya kupanua serikali ni hatua ambayo inastahili kuungwa mkono kwa kuwa ni njia mojawapo ya rais Kenyatta kuliunganisha taifa .

“We, therefore, wish to commend and thank the President for taking this bold move, especially at this time when the whole world and the country is fighting the devastating Covid-19 pandemic,”  Imathiu amesema.

Bila ya kuzungumzia mbadiliko yanayofanyika katika chama tawala cha Jubilee, Gema imesema kuwa watampatia uungwaji mkono kuhusiana  na hatau hiyo.

“We are aware that there will be heated political discourse on the actions that his excellency the President is taking, particularly within the political parties and government,” Imathiu amesema.

Kupitia kwa Imathiu, Gema imesema kuwa inapania kuwasilisha mapendekezo yake katika kamati kuu ya jopo la maridhiano ya BBI.

“We believe that the President's agenda will provide the country with the blueprint for unity, avenues for resolving weaknesses in the Constitution, governance and removing corruption from among and within Kenyan institutions,” Imathiu aliongezea.