Kenya yasajili visa 22 zaidi vya coronavirus na kufikisha jumla ya visa 1,214

Rashid Aman
Rashid Aman
Visa vya ugonjwa wa COVID 19 nchini  vimeongezeka   hadi  1,214 baada ya visa  22 zaidi vya ugonjwa huo kuripotiwa katika kipindi cha saa  24 zilizopita .

Hii ni kutoka sampuli 1,108  zilizopimwa na kufikisha jumla ya sampuli 59,260 hadi kufikia sasa

Mgonjwa zaidi ameaga dunia  na kufikisha 51 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo hadi kufikia sasa .

kati ya visa hivyo 22 17 ni wanaume ilhali 5 ni  vya wanawake . Wagonjwa walioathiriwani kati ya umri wa miaka 24-73.

katika visa hivyo vya leo Nairobi (10), Mombasa (9), Kwale ( 1), Nakuru (1), Taita Taveta(1).

katibu wa utawala wa wizara ya Afya  Rashid Aman  amesema watu wengine watatu wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha 383 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo .

Aman amewashauri wakenya kuendelea kutii maagizo  yaliyotolewa na wizara ya afya  ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hivyo .Amewapongeza wakaazi katika maeneo yalio chiniya maagizo ya kutotoka nje kwa kushirikiana kikamilifu  na serikali .Pia amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi ili kupimwa virusi vya corona