Sabina Chege atoa msaada wa chakula kwa makahaba

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Murang'a Sabina Chege amewapa msaada wa chakula zaidi ya makahaba 100 na kuwafanya wafurahie sana.

Kupitia ukurasa wa Facebook, Chege alisema makahaba hao walimuelezea kuwa janga la virusi vya corona limeathiri sana biashara yao na hata kufanya wakose chakula.

"Kundi kadhaa la wanawake wanaofanya biashara ya ngono kupitia kwa mwenyekiti wao waliniomba msaada wa chakula wakidai hali ngumu ya maisha na kwamba janga la corona limeathiri biashara yao." Aliongea Sabina.

Chege alisema chakula hicho kitawatosheleza makahaba hao kwa muda wa juma moja na ataendelea kuwasaidia hadi hali iwe nzuri. Ni virusi ambavyo vimeathiri uchumi wa nchi hasa kwa wafanyabiashara wa hali ya chini.

" Tumeafikiana na makahaba hao kuwa tutatafuta suluhu la kudumu ambalo litawasaidia hao kupata chakula kwa urais na kuahidi kuasi biashara hiyo na kufanya biashara nyingine kama ya saluni na ya kushona nguo." Aliongea Sabina Chege.

Swali ambalo linazidi kugonga vichwani mwa wananchi ni je, hali ya kawaida itarudi lini na mambo yatakuwa sawa lini licha ya janga la corona na nchi kurekodi visa vipya kila siku.