'Unakuanga umeweza,'Betty kyallo akiri upendo wake kwa Redsan

redsan
redsan
Mwanahabari Betty Kyallo amesema mtu mashuhuri anayemmezea mate ni msanii Redsan. Akizunguza kupitia mitandao ya kijamii ya youtube akiwa na dada yake na binamu yake aliwapa changamoto wataje watu wanaowamezea mate.

Betty alisema amekuwa akimmezea mate msanii wa nyimbo za raggae na dancehall Redsan kwa muda mrefu sana.

“I HOPE HE DOESN’T WATCH THIS, BUT HE IS MY CRUSH. THERE IS A TIME I INTERVIEWED HIM IN ELDORET AND I WAS LIKE, YOU GUY! YOU KNOW, THERE IS A WAY HE JUST SITS AND LOOKS AT YOU, YOU KNOW HE IS LIKE, EEH." Betty Alisema.

Betty aliongeza na kusema kuwa kumezea mtu mate haimaanishi kuwa atakuja kuwa mpenzi wako na anashukuru na anatamani Redsan awe tu akimmezea mate.

“REDSAN, MANZE, UNAKUANGA UMEWEZA, BRO,” Betty Alisema.

Aliwashauri pia wanadada wawahusishe dada wenzao katika bishara zao ili wajue mengi.

"Ni muhimu wajue kazi yako na kisha wajifunze kujisimamia kimaisha, wapeleke kujivinjari si kuwa tu pekee bali wajue pale pesa zako hutoka." Alizungumza Betty.